Mafunzo ya Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mpango Mkakati
Katika kipindi cha miaka kumi, Tanzania imepiga hatua kubwa katika utambuzi, uratibu na uingizwaji wa mifumo ya ufuatiliaji na tathmini kwenye taasisi na mashirika ya umma. TSSL imeandaa programu maalum ya kujenga uwezo wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa sera, mipango, mikakati na miradi. Programu hii inatoa mafunzo ya ana kwa ana ya wiki moja, yakifuatiwa na kipindi cha uelekezi na ushauri wa karibu kupitia majukwaa ya mtandaoni na simu.
⬇ Pakua Brochure🎯 Malengo ya Mafunzo
- Kusanifu mfumo madhubuti na wenye ufanisi wa ufuatiliaji utekelezaji wa mpango mkakati
- Kuandaa na kutekeleza mpango madhubuti wa ufuatiliaji utekelezaji wa mpango mkakati
- Kuandaa na kutekeleza bajeti za ufuatiliaji utekelezaji wa mpango mkakati
- Kuandaa nyenzo za kukusanya data kwa kutumia mbinu mseto
- Kukusanya, kuchakata na kuchanganua data za ufuatiliaji
- Kuandaa taarifa za ufuatiliaji za kiwango cha juu
- Kusambaza taarifa za ufuatiliaji utekelezaji wa mpango mkakati
👥 Walengwa wa Mafunzo
- Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Ufuatiliaji na Tathmini
- Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Mipango
- Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Miradi
- Wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini
- Wadau wengine wa Ufuatiliaji na Tathmini
📚 Mada Kuu
- Mada 1: Misingi mikuu na umuhimu wa ufuatiliaji utekelezaji wa mpango mkakati
- Mada 2: Jinsi ya kuandaa mfumo, mpango na bajeti ya ufuatiliaji
- Mada 3: Jinsi ya kuandaa nyenzo za ufuatiliaji utekelezaji wa mpango mkakati
- Mada 4: Jinsi ya kukusanya data za ufuatiliaji
- Mada 5: Jinsi ya kuchakata na kuchanganua data za ufuatiliaji
- Mada 6: Jinsi ya kuandaa taarifa za ufuatiliaji
- Mada 7: Jinsi ya kuwasilisha na kusambaza taarifa za ufuatiliaji
📅 Tarehe za Mafunzo
🧭 Njia ya Mafunzo
Mbinu shirikishi na ya kivitendo inayojumuisha wiki moja ya mafunzo ya ana kwa ana, ikifuatiwa na uelekezi na ushauri kwa njia ya barua pepe, WhatsApp na simu. Mafunzo yatatumia mfumo wa TSSL wa Kujifunza, Kujaribu na Kutenda (K3).
📍 Sehemu ya Mafunzo
Hoteli ya Morogoro iliyopo katika Manispaa ya Morogoro. Ukumbi huo unatoa mazingira wezeshi na upo karibu na vivutio vya asili kwa ajili ya utalii na mapumziko.
Ada ya Ushiriki
Ada ya usajili kwa kila mshiriki ni TZS 950,000. Ada hii INAJUMUISHA gharama za vitini, chai (asubuhi na jioni) na chakula cha mchana wakati wa mafunzo, lakini HAIHUSISHI gharama za usafiri na kujikimu. Mwisho wa usajili ni siku 7 kabla ya kuanza kwa mafunzo.
📝 Jinsi ya Kujisajili
- Chagua kundi la kushiriki
- Pakua fomu ya usajili kutoka kwenye tovuti yetu
- Jaza fomu
- Omba ankara ya malipo
- Fanya malipo ya ada kupitia tsslevents@gmail.com au WhatsApp 0754 300143
- Wasilisha fomu iliyojazwa na uthibitisho wa malipo kupitia barua pepe tsslevents@gmail.com au WhatsApp 0754 300143
